Web

Wasanii Jifunzeni Kupitia Anguko la Mo Music Kimuziki....



Hii #clip ambayo Mo Music yupo juu ya gari ina-trend sana kwenye Mitandao ya kijamii, Watu wengi wamesikitishwa sana na Clip hiyo kwani imethibitisha kwa namna gani Mo Music ameshuka kimuziki.

Hapo ni Kasulu, Kigoma, Mo Music alikuwa anatumbuiza Tarehe 28 Februari 2025, hivyo hapo wanazunguka mtaani ku-promote show, anayetangaza sasa anawaambia Watu Wamtazame mtu aliyekaa juu ya Gari aliyevaa T-shirt ya njano anaitwa #MoMusic, Kiingilio ni Elfu Tano tu. Pata picha Mo Music enzi hizo alikuwa ana Hits kibao kama #BasiNenda #Bajaji #Skendo #Nitazoea ila leo anatambulishwa Vijijini kama Mtu asiyejulikana na anafanya show kwa Kiingilio cha Elfu Tano!

Mo Music amewahi kufunguka kuwa chanzo cha kushuka kimuziki ni pale ambapo alitofautiana na Management yake kisha akaanza kufanya kazi kwa kujitegemea, hapo kila kitu kilienda vibaya akasimama kwa zaidi ya miaka 4 bila kutoa ngoma, mtaani story zilikuwa nyingi mara jamaa ni mlevi sana. Mwaka 2018 nakumbuka amewahi kukumbwa na Skendo ya kupewa busha baada ya kumdhulumu #Promoter, yaani alilipwa pesa lakini hatutokea kwenye show, kiufupi hapa kati kati amepitia mengi mpaka kuna mahojiano alifanya mwaka jana akasema kwamba hataki tena kufanya muziki.

Mo Music ni Sample tu lakini Wasanii waliopotea angali bado wana uwezo mkubwa ni wengi sana, hivyo wasanii wanaofanya vizuri sasa #wasibweteke, wajue kwamba kuna kupotea kwenye game hivyo wajitahidi kuziheshimu Management zao, pia wawekeze kwenye biashara kama #DiamondPlatnumz #Harmonize #Alikiba #Jux ili Muziki ukikata wawe na mchongo mwingine sio tena kupiga Show za Chaka kwa Chaka..

#hopetygatz

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad