Winga wa klabu ya Orlando Pirates ya Afrika kusini Monnapule Seleng ametajwa na vyombo vya habari nchini humo kuomba kufikia tamati ya mkataba wakuitumikia timu yake mwishoni mwa msimu huu.
Winga huyo ambaye amekosa furaha baada ya kuanza kusugua benchi ametajwa kuwindwa na vigogo mbalimbali Afrika kama Simba na Yanga pia na timu zingine kutoka Libya.
Pirates wanatajwa kupokea maombi ya Seleng na kuyakataa huku pia Ofa kutoka timu zinazomhitaji zikifingwa milango.
Mkataba wa Seleng na Pirates unamalizika mwishoni mwa msimu wa 2026.