Web

Yanga: Hatupo Tayari Kupangiwa Kucheza Derby Siku Ingine zaidi ya Leo






Licha ya klabu ya Simba kutoa tamko la kususia kuleta timu uwanjani kwenye mchezo huo wa derby ya Kariakoo uliopangwa kuchezwa leo Machi 8, 2025 kufuatia kikosi chake kuzuiwa kufanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetoa tamko kwamba mechi hiyo ipo palepale kama ilivyopangwa.

Mwenyekiti wa TPLB, Steven Mnguto amesema licha ya Simba Sc kudai haitaleta timu mchezo huo upo palepale huku akibainisha kuwa TPLB imesikia matukio yote na inafuatilia kuanzia hatua ambayo yalijiri na tayari inafanyia kazi ripoti za awali ambazo zimepokelewa kutoka kwa wasimamizi mbalimbali.

“Kwanza niwatoe wasiwasi mashabiki wa soka na wadau kwa ujumla. Mchezo upo palepale kama ambavyo kalenda yetu ya soka inavyosema, hakuna mabadiliko yoyote, mashabilki wajipange kuja kutazama mchezo.”——amesema Mnguto

“Nimeitisha hiki kikao cha haraka kitafanyika asubuhi hii. Bahati mbaya sitaweza kushiriki, lakini nimemuagiza makamu wangu akisimamie tujadili matukio haya yaliyotokea jana na hii taarifa ya Simba’ ——ameongeza

“Tutatoa taarifa kamili mapema sana kwenda kwa wadau wote. Kwa hiyo tunaomba watu wawe na subira, lakini kama nilivyosema mchezo upo kama ambavyo umepangwa hakuna mabadiliko. Hayo mengine tutayatolea ufafanuzi zaidi mara baada ya kikao kukamilika.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad