Web

Yanga Kupimana Nguvu na Rayon Sports Uwanja wa Amahoro Rwanda



Rais wa Rayon Sports, Twagirayezu Thaddée, amethibitisha kuwa Yanga SC ya Tanzania, iko tayari kucheza nao kwenye Uwanja wa Amahoro kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu.

Twagirayezu amesema pia kuipeleka timu ya Rayon Sports katika uwanja wa Amahoro ni mojawapo ya tathmini ambayo waliifanya kama uongozi ili kuhakikisha msimu wa 2025/26 unazaa matunda.

Pia alifichua kuwa ili kuendelea kuongeza tija, kumekuwepo na mazungumzo kati ya Rayon Sports na Rais wa Young Africans Sports Club (Yanga SC), Hersi Said ambaye ameeleza nia yake ya kucheza katika uwanja huo, timu zote mbili zitacheza mechi mbili za kirafiki.

Rayon Sports chini ya kocha Robertinho kwasasa ndiyo inayoongoza kwenye msimamo wa Ligi Kuu Rwanda ikiwa inapewa nafasi ya kutwaa kombe msimu huu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad