Kamati ya Utendaji ya Yanga, chini ya Rais wake Eng. Hersi Said imefanya Kikao cha dharura leo March 9, 2025 kwa njia ya mtandao ambapo imetoa msimamo wa kutaka ipewe haki yake ya ushindi kama inavyoelezwa kwenye kanuni, pindi timu moja inapogomea mechi lakini imekubaliana kutoshiriki mchezo namba 184 dhidi ya Simba kwa tarehe yoyote itakayopangwa.
Klabu hiyo imesema kutokana na mfululizo wa uvunjifu na kushindwa kusimamia kanuni za Ligi Kuu, imekosa imani na Kamati ya Uendeshaji ya Ligi Kuu, chini ya Mwenyekiti wake Steven Mnguto na Katibu wa Kamati hiyo Almas Kasongo, hivyo imeliomba Shirikisho la Mpira wa miguu - TFF kuivunja kamati hiyo na kuteua Viongozi wengine waadilifu na wenye nia njema kwa maslahi mapana ya mpira wetu.
“Tunawaomba Wanachama, Wapenzi na Washabiku wa Yanga kote duniani kuendelea kuwa watulivu wakati Uongozi ukiendelea na taratibu za kuhakikisha kuwa sheria na taratibu za uendeshaji wa mpira wa miguu, na harakati za kudai haki yetu zikiendelea”