Anaandika Jemedari Saidi mchambuzi wa masuala ya kandanda wa Crown Fm.
"Katika malalamiko hayo Rasmi kwa bodi ya ligi licha ya kuomba alama 3, wanataka walipwe gharama zote za maandalizi ya mchezo ambazo ni Tshs 56,435,000 ambazo zimeanishwa katika kipengele namba 17 cha barua hiyo yenye vipengele 19.
"Katika kipengele namba 18 wanasisitiza kwamba wanataka ifahamike wazi hawako tayari kuicheza mechi hiyo katika msimu huu. Na kwamba mechi ilighairishwa kwa makosa ya makusudi ya Simba SC kwahiyo wanastahili alama 3.
"Wameipa Bodi ya ligi masaa 72 baada ya kupokea barua yao kutoa maamuzi ya haki na weledi kwa kuzingatia madai yao.
"Mwisho wanasema kama madai yao ya alama 3 na mabao 3 na gharama za mchezo hayatozingatiwa na kupewa umuhimu wa kupata haki yao, watalipeleka suala hili kwenye mamlaka za juu zaidi. Nifuate