Haji Manara amefunguka kua klabu ya Yanga itaenda CAS kwa ajili ya kufungua kesi kudai Haki Yao ambayo imechukuliwa wakati wa mchezo wao na Simba wa March 8. Manara ameongeza pia katika kuendesha kesi hiyo atahakikisha wana yanga Wote wanachanga wakiweko mashabiki wa kawaida na wanachama wenye Kasi.
Haji amesisitiza Zaidi kua kiasi cha Shilingi Millioni 150 au 300 sio shida kwa wanachama wa klabu ya Yanga na hataki bajeti ya timu kutumika kwa ajili ya kesi hiyo. Na sasa mechi ya tarehe 8 inazidi kuchukua sura mpya kila kukicha.
Utaratibu Wa CAS Utakuwa Hivi
Yanga walitakiwa kutoa masaa 72 ikiwa Watapata faida ya Pointi 3 na magoli matatu baada ya timu ngeni ( Simba. ) Kushindwa kufika muda wa mechi. Hivyo ikiwa TFF hawajafika matakwa hayo Yanga Haki Yao Watapata CAS.
Huko CAS vita itakuwa kati ya Yanga na bodi ya ligi kwanini? Simba wamefuata taratibu mechi ilitangazwa kufutwa na bodi ya ligi yenyewe hapo Simba itakuwa nje ya sakata. Yanga watabaki na vita na Bodi ya ligi chini ya TFF.
Swali ni je TFF walitumia busara au Sheria kuahirisha mchezo, ni kweli Yanga wameajiri Baunsa kwa ajili ya kulinda uwanja?. Kwa misingi ni kua TFF wanaweza kuthibiti kua kweli Simba walifanyiwa vitendo ambavyo sio vya kiungwana lakini sio Sababu kuahirisha mchezo.
Ila shida kubwa kwa Bodi ya ligi ni kuahirisha mechi, kawaida mechi inatakiwa kuchezwa kwanza na baada ya hapo timu inayolalamika kufika kwa ajili ya taratibu za kisheria. Na kikao ni masaa 72 baada ya mchezo lakini bodi ya ligi ilitoa taarifa asubuhi mechi ipo alafu mchana ikafuta mechi. Tusuburi tuone.
From Opera News
Maudhui yaliyoundwa na kutolewa na Quodare0314