Ameandika dericklissu
Sajili yake ilikuwa ya kisiasa na ya kibiashara, mahitaji ya timu hayakuhitaji mchezaji wa aina yake. Lakini bado, alitengeneza hype kubwa akawa headline ya dirisha kubwa la usajili! Story yake ilizima kila sajili nyingine kwenye dirisha kubwa, Hakukuwa na story zaidi ya jina lake.
Lakini sasa, Mwamba wa Lusaka hana furaha na maisha ya Jangwani. Sauti za kurejea Msimbazi zinasikika tena kwa nguvu. Inawezekana, safari yake haijaisha…
Mashabiki wa Simba, mpo tayari Mwamba wa Lusaka avae tena jezi nyekundu?
Chama alisaini mkataba wa mwaka mmoja na Yanga, mkataba huo unamalizika rasmi mwezi Juni. Hadi sasa, kikanuni anaruhusiwa kuzungumza na timu yoyote na hata kusaini mkataba wa awali.
Furaha na matamanio yake ni kurejea Msimbazi mahali alipotengeneza ufalme wake nchini na kuandika historia kubwa, hali iliyopo Jangwani haimpi tena furaha
Kwa heshima na taadhima, naomba niwasihi viongozi wa Simba SC: mumpe “One Last Dance” Mwamba wa Lusaka. Tumkaribishe tena Chama pale alipoacha alama isiyofutika.
Chama alisaini mkataba wa mwaka mmoja na Yanga. Katika mkataba huo, anapokea zaidi ya dola 200,000 kama signing fee. Tayari amelipwa dola 120,000, huku nusu ya pili ikisubiriwa kukamilishwa.
Kiufupi, Yanga imetumia zaidi ya milioni 500 za kitanzania kumsajili Mwamba wa Lusaka kwa mkataba wa mwaka mmoja tuu!