Klabu ya Yanga Sc imefungua kesi ya malalamiko kwenye Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) hatua inayokuja baada ya kutoridhishwa na majibu ya Shirikisho la soka Tanzania TFF kufuatia kuahirishwa kwa mchezo wa Dabi ya Kariakoo.
Kwa mujibu wa ripoti Wananchi hawana imani na bodi ya ligi na wameshindwa kukubaliana kabisa na majibu ya barua iliyotoka na hivyo wameamua kusonga mbele (CAS) ili kudai haki.