Web

Zelensky: PUTIN Atakufa Muda Wowote Kuanzia Sasa

Top Post Ad

Zelensky: PUTIN Atakufa Muda Wowote Kuanzia Sasa


Rais wa Ukraine, #VolodymyrZelensky, amedai kwamba Rais wa Urusi, #VladimirPutin, "atakufa hivi karibuni" huku kukiwa na tetesi kwamba afya ya kiongozi huyo wa Urusi inazorota.

Zelensky alitoa kauli hiyo katika mahojiano na waandishi wa habari jijini Paris baada ya kukutana na Rais wa Ufaransa, #EmmanuelMacron. Alisema: "Putin atakufa hivi karibuni, na hilo ni jambo la uhakika."

Picha za Putin zilizochunguzwa kwa muda zimezua uvumi kuhusu hali yake ya afya, hasa baada ya kuonekana na macho mekundu na alama ya ajabu kwenye mkono wake. Aidha, picha zingine zimeonyesha kovu shingoni mwake, likizua dhana kwamba huenda alipitia upasuaji wa saratani ya tezi dume.

Ripoti za awali zilidai kuwa Putin alikuwa akifuatana mara kwa mara na daktari bingwa wa saratani, huku uvujaji wa taarifa za kijasusi za Marekani ukionyesha kuwa alikuwa akipokea tiba ya saratani. Vilevile, amekuwa akionekana akiwa na miguu isiyo imara, akishika meza kwa nguvu, au akitikisa mguu wake mara kwa mara, hali inayoongeza mashaka kuhusu afya yake.

Below Post Ad

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.