Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga SC Ali Kamwe amevunja ukimya wake baada ya taarifa kusambaa katika mitandao ya kijamii zinaonyesha kuwa kipa wa klabu ya Fountain Gate aliuza mechi yao dhidi ya Young Africans. Nikinukuu maneno ya msemaji wa klabu ya Yanga SC Ali Kamwe: makolo hii mliuza bei gani?
Kipa kutoka Nigeria John Noble ambaye ni kipa wa timu ya Fountain Gate na timu ya taifa ya Nigeria amefukuzwa kwenye klabu hiyo baada ya makosa ya wazi kwenye mchezo wa leo dhidi ya Young Africans.
Habari za uhakika zinasema kuwa Noble aneshaondolewa kambini na hayupo na wenzie. Aliondoka kiwanjani baada tu ya kufanyiwa mabadiliko huku wenzie wakitaka Kumpiga kwa makosa hayo ya kijinga.
Aidha Kocha Mkuu wa klabu ya Fountain Gate ametema cheche baada ya mechi ya leo na kudai kuwa mchezaji huyu alisababisha wao kupokea kichapo kikali cha mabao 4-0 dhidi ya Young Africans leo.
Kulingana na taarifa tulizozipata hivi sasa Kocha Mkuu wa klabu ya Fountain Gate, Robert Matano alizungumza na waandishi wa habari mara tu baada ya mechi ya leo ya Fountain Gate dhidi ya Young Africans kukamilika.
Alisema kuwa golikipa wao aliwaangusha kabisa. Alieleza kuwa golikipa alifanya makosa mengi ambayo yalisababishwa kupata kichapo kikali. Jambo ambalo huenda likawa pigo kubwa kwa mchezo huyo.