Kwa mujibu wa Mtangazaji Mwijaku ambaye yupo karibu sana na Alikiba ametoa taarifa kuwa Alikiba amevunja Mkataba na Meneja wake (Aidan), inadaiwa kabla ya kuvuliwa umeneja alivuliwa Ukurugenzi Utendaji (CEO) wa media ya Alikiba. Mpaka sasa haijulikani kwanini Alikiba amemtema Aidan kwenye nafasi hizo mbili.
Kwa upande wa Mwijaku ametangaza kwamba ameacha uchawa, hivi sasa ana mpango wa kupeleka CV awe Meneja mpya wa Alikiba. Ikumbukwe miezi kadhaa nyuma Phina pia aliachana na Meneja wake wa muda mrefu D Fighter, vipi unadhani kipi kinaweza pelekea Msanii kuvunja mkataba na Menejimenti yake?