Kati kati ya Fullback na center back (half-space) kuna nafasi….yes! kati kati ya Meza na Msindo kuna shimo Dube kama namba tisa alitakiwa kufanya mikimbio ya kuchongwa ili kupokea mipira na kusababisha hatari kwenye lango la Azam.
Leo amefanya hicho kitu mfululizo tena kwa mafanikio makubwa✍️
Rejea mikimbio yake kwenye goli la kwanza ambalo ame-assist kwa Pacome🔥
Dube ni runner na leo aliwapa wakati mgumu Azam Fc.
Goli lake ambalo ni la pili kwa Yanga lilikua tamu ila ile Assist kwa Pacome ilikuwa hatari zaidi…kila kitu kilikua on point🔥
Dube amehusika kwenye goli (20) msimu huu (the most) ana goli (12) na assist (8).
Another Super performance kutoka kwa Baby Face Prince Dube