Kuna namna Yangasc wametupatia funzo ambalo linakwenda kubadilisha moja kwa moja muundo na mtindo mbovu wa uendeshaji wa ligi yetu
‎
‎Alikuwa anangojewa shujaa mmoja mwenye nguvu kulifanya hili na hakuna mwengine zaidi ya hawa vijana wawili wenye maamuzi na soka leo Yangasc wamekua waanga wa kwanza wa kudai kanuni na sheria kwenye ligi
‎
‎ingekuwa aibu kwenye taifa letu kuwa na watu wakubwa wenye nyadhifa kubwa kwenye shirikisho la mpira wa miguu Afrika CAF
‎
‎Ni aibu tungeendelea kukubali busara kuwa sheria huku kanuni na taratibu ziwe kwa Kagera Sugar na Mtibwa sugar hali ya kuwa kwenye hili taifa tuna mwenyekiti wa vilabu barani Afrika
‎
‎kama sio Hersi Said kusimama kidete kwenye kuzilinda klabu zote Afrika ni nani mwengine
‎
‎ukiangalia kwenye hili sakata Rais wa Yangasc amekuwa akivaa kofia mbili kubwa kwenye soka la Afrika hivyo kama atashindwa kutatua changamoto ndogo kama hii ambayo ipo nyumbani kwake je likitokea kwa Al ahly itakuwaje
‎
‎Itoshe kusema kua mpira bila ya busara inawezekana.