Kiungo Azizi Andabwile ambae yupo kwa mkopo wa mwaka mmoja Yanga SC akitokea Singida Black Stars ameshikilia msimamo wake wa kuvunja mkataba wake na waajiri wake Singida BS.
Kesi yake ya kuvunja mkataba ipo shirikisho la soka nchini TFF na bado haijasikilizwa baada ya Singida Black Stars kutofika kwa madai kuwa walibanwa.
Andabwile bado anadai fedha zake za usajili (Signing Fee) anawadai Singida Black Stars japo pia aliahidiwa fedha hizo atalipwa na Yanga SC.