BREAKING NEWS: Rasmi Yanga wameingilia kati dili la Fei Toto
Jioni ya leo viongozi wa Yanga wamefanya mazungumzo na wawakilishi wa kiungo huyo wa Azam ili kumshawishi arejee Jangwani.
Chanzo changu kimeniambia ofa ya Yanga (sign-on fee) ni kubwa kuliko ya Simba.
Mwishoni mwa msimu huu Yanga wanatarajia kumuuza Aziz Ki,lakini bado Pacome hajasaini mkataba mpya hivyo Yanga wanamuona Fei kama mbadala sahihi.
Mpaka sasa Fei ana ofa tatu tofauti kutoka nchini.
1. Ofa ya mkataba mpya kutoka Azam.
2. Ofa kutoka Simba.
3. Mega ofa kutoka Yanga.
Pingamizi pekee la Fei kurudi Yanga liko kwa Mama yake mzazi ila taarifa zinasema Yanga wako tayari kuchutama na kuomba msamaha.