CAS Yapokea Barua ya Yanga SC Yawapa Siku 10 TFF, TPLB na Simba
Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) imepokea rasmi rufaa iliyowasilishwa na Klabu ya Young Africans SC dhidi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) na Klabu ya Simba kufuatia uamuzi uliotolewa TPLB wa kuahirishwa derby ya Kariakoo iliyotakiwa kupigwa Machi, 8 2025.
Kwa mujibu wa barua ya CAS walalamikiwa, TFF, TPLB na Simba wamepewa siku 10 kuanzia tarehe ya kupokea taarifa hiyo ili kuandaa na kuwasilisha utetezi wao.
Kesi hiyo itasikilizwa kwa haraka chini ya kumbukumbu namba CAS 2025/A/11298 huku pande zote zikitarajiwa kuwasilisha vielelezo na hoja zao ndani ya muda uliopangwa.