Web

Chadema Imejiondoa Rasmi Kushiriki Uchaguzi Mkuu?


Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Ndugu John Mnyika ameufahamisha umma kwamba hatohudhuria na hatoshiriki kwenye kikao cha leo Aprili 12, 2025 kilichoitishwa na Tume huru ya Taifa ya uchaguzi kikihusisha vyama vyote vya siasa vitakavyoshiriki kwenye uchaguzi Mkuu ujao kwaajili ya kusaini kanuni za maadili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Kulingana na Taratibu, wawakilishi wa vyama vya siasa katika Kikao hicho wanatakiwa kuwa Watendaji wakuu wa Vyama (Makatibu wa vyama), kwakuwa ndio wenye mamlaka ya kusaini maadili hayo ya uchaguzi mkuu.

"Katibu Mkuu sijateua kiongozi ama afisa yeyote kwenda kushiriki kwa niaba yangu katika kikao hicho kitakachofanyika kwenye Ofisi za Tume ya Taifa ya uchaguzi Mkoani Dodoma."imesomeka taarifa ya John Mnyika.

Wakati hayo yanafanyika ikumbukwe kuwa Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu ametiwa korokoroni, wakati ambapo Makamu wake mwenyekiti John Heche kupitia kurasa yake ya x amechapisha taarifa akieleza malalamiko yake kadhaa ya kutokuwa na imani na tume hiyo na kile ambacho wametangaza kukifanya hii leo.

"Tume ya Taifa ya uchaguzi nchi hii haijawahi kuwa na maadili, ni tume ambayo inakisaidia Chama Cha Mapinduzi, haiwezi kuwaambia watu wasaini maadili, kwasasa hoja ni moja tu No Reforms, No election", amesema.

Jana kulingana na taarifa ya Tume ya uchaguzi iliyochapishwa na JamboTv, Mkurugenzi wa uchaguzi wa Tume huru ya Taifa ya uchaguzi Bw. Ramadhan Kailima alisisitiza kuwa Chama ambacho alithibitisha kuwa Chama cha siasa kitakachokwepa kusaini kanuni hizo za uchaguzi, hakitaruhusiwa kushiriki kwenye uchaguzi mkuu kwani maadili hayo yamendaliwa kwa mujibu wa sheria za uchaguzi.

Kusainiwa kwa kanuni za maadili kunakuja wakati huu ambapo Chadema imeendelea kusisitiza kuhusu kampeni yake ya No reforms, No election, wakitanabaisha kuwa bila mabadiliko ya kisheria, hakuna uchaguzi na kulingana na kauli ya Katibu Mkuu wa Chama hicho na taratibu za Tume ya Uchaguzi.

Swali kubwa sasa ni kuwa Chadema ndiyo wamejiondoa rasmi kwenye uchaguzi Mkuu ujao?Nini hatma ya Chama hicho na vuguvugu lililoanzishwa na kundi la G55?

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad