"Chama chatu (CHADEMA) kisiposhiriki uchaguzi kitapoteza mvuto, kitapoteza mvuto kwa sababu mfano mikutano inayoendelea sasa hivi (inayofanywa na viongozi wa CHADEMA na vyama vingine), hii ni mikutano ya kawaida, lakini tukiwa kipindi cha kampeni mikutano yake inakuwa ya sera, watu wengi wanakuja kusikiliza sera zetu kipindi cha kampeni, kwahiyo kipindi cha kampeni ni muhimu sana cha kukiimarisha chama kupitia mikutano ya hadhara, kwa sababu mnapokuwa na mgombea Urais, wagombea Ubunge na wagombea wa Udiwani hawa wote wananadi sera zenu" -Ntobi
"Lakini la pili, kama tunashiriki na ndani yake tunaweza shinikizo la kuuzuia watu wataona kweli namna mnavyopambana, kisha watawiwa kuwaunga mkono maana wameona jinsi mlivyonadi sera zenu, mmeeleza matatizo yao, mmeeleza muelekeo wenu, mmesema changamoto zao kama vile za barabar, maji nk pale unapolalamikia jambo, au unapokuja kusema nimekatwa watu wengi sana watawaunga mkono, sasa tukikaa kimya tukakosa hizo siku 60 zote za kampeni ni sawa na hamna chama, tusiposhiriki hamna sera ambazo watu watazisikiliza" -Ntobi
"Ukisoma maazimio ya tarehe 21/01/2025 (wakati wa mkutano mkuu wa CHADEMA) tuliambia na Katibu Mkuu (John Mnyika) kwamba endeleeni, pamoja na kwamba tunapambana kudai reforms, lakini tusiache kuendelea kuandaa wagombea kwa ngazi zote, hiyo maana yake ni kwamba tuanze kuandaa ilani ya kwetu ya uchaguzi ambayo tukija sasa hivi (mfano hawa CCM wamekuja na slogan yao wanasema 'Kazi na Utu') sasa na sisi (CHADEMA) tungekuja na slogan yetu kama tulivyofanya mwaka 2015 au mwaka 2020, kitu ambacho kinawafanya watu wazidi kuamini kwamba hawa watu ni wa watu, kwahiyo tunazidi kuwa na 'vibe' hata bila kuwa na Mbunge" -Ntobi
Ni sehemu ya yale aliyozungumza aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga Emmanuel Ntobi alipokuwa akihojiwa na East Africa radio kupitia kipindi cha Supa Breakfast mapema leo, Jumanne Aprili 15.2025