Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Ramadhani Kailima amesema chama ambacho hakijasaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi leo hakitaruhisiwa kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huu na chaguzi zote zitakazitokea katika kipindi cha miaka mitano ikiwemo uchaguzi mdogo.
Akitoa ufafanuzi huo baada ya vyama 18 Kati ya 19 vyenye usajili wa kudumu kusaini kanuni hizo Katika ofisi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Kailima amesema vyama vyote vilipewa taarifa kwa maandishi na kwa kupigiwa simu na wote walipokea taarifa ya tukio hilo.