Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar Saidi Issa Mohammed na wenzake watatu (3) wamefungua kesi namba 8323 ya mwaka 2025 dhidi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiiomba Mahakama kutoa amri ya kusimamisha shughuli zote za kisiasa zinazoendelea ndani ya chama hicho hadi hapo kesi yao itakaposikilizwa na kutolewa maamuzi
Inaelezwa kuwa kesi hiyo iliyofunguliwa kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam imeitwa leo, Alhamisi Aprili 17.2025 chini ya Jaji Hamidu Mwanga
Katika hatua nyingine, baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wadhamini wa chama hicho wamefungua kesi dhidi ya chama chao wakidai kuwa katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za chama Zanzibar imekuwa ikitengwa
Akihojiwa na Jambo TV kwa njia ya simu mapema leo, Alhamisi Aprili 17.2025 Mwanasheria Mkuu wa chama hicho Dkt. Rugemeleza Nshala amethibitisha uwepo wa shauri hilo Mahakamani, ambapo amesema wanachama hao wapo watatu na madai yao makubwa ya msingi wanasema CHADEMA imekuwa ikiitenga Zanzibar katika matumizi ya mali za chama.