Web

Dawa ya Upara Yagundulika Ngorongoro

 

Dawa ya Upara Yagundulika Ngorongoro

Upara ni hali ya kutokuwa na nywele au ukosefu wa nywele mahali ambapo mara nyingi hukua, hasa kichwani aina ya upara ya kawaida zaidi ni upungufu wa nywele unaowatokea hatua kwa hatua binadamu wanaume.


Na mwandishi wetu.


Taasisi ya utafiti wa wnyamapori Tanzania (TAWIRI) imetangaza ugunduzi mpya wa dawa ya asili ya inayoweza kuotesha nywele na kuzuia nywele kukatika.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, hii leo April 22,2025 mkurugenzi wa utafiti kutoka TAWIRI, Dkt. Julius Keyyu, amesema kuwa dawa hiyo ambayo ni matokeo ya utafiti wa miaka 12 imeonesha uwezo wa kipekee katika kuotesha nywele na kuzuia upara.


Amesema ugunduzi huo kwa mujibu wa TAWIRI ni kupitia utafiti wa mimea ya tiba asili uliofanywa tangu mwaka 2013 katika wilaya za Ngorongoro,Mbulu na Hanang kwa lengo la kugudua dawa au vipodozi ambavyo vinaweza kutumika kwa binadamu .


Katika ugunduzi wa kwanza wa dawa ya kuotesha nywele kwa watu wenye upara imetokana na magome ya mti ulioko wilaya ya Ngorongoro unaojulikana kama Mporojo au kwa kitaalamu Albizia anthelmintica.


Ameongeza kuwa utafiti huo wa kusaka mimea yenye uwezo wa tiba za asili ulihusisha jamii za kimasai, hadzabe, datoga na Iraq na umefanikisha kupata matokeo mazuri.


Ameongeza kuwa hii ni habari njema kwa watu wenye vipara au nywele zisizoota na pia wale wenye nywele zinazokatika hovyo, utafiti wa kisayansi umeonesha mmea huu una uwezo wa kipekee katika kuchochea ukuaji wa nywele na kuzuia kipara.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad