Mtumsimi wa Mungu Boniphace Mwamposa ametoa taarifa njema kwa mashabiki na wadau wa klabu ya Simba Sc mara baada ya kuhusishwa na taarifa za kupewa mualiko wa kuwa mgeni maalumu kwenye mchezo ujao ambao watacheza dhidi ya klabu ya Al Masry.
Simba Sc watakuwa wenyeji kwenye mchezo huo ambao utapigwa siku ya Jumatano tarehe 9 Aprili, katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam majira ya Saa 10:00 jioni kwa masaa ya Afrika mashariki.
Kuelekea katika mchezo huo, siku ya jana Jumamosi tarehe 5 Aprili klabu ya Simba Sc kupitia kwa afisa hawana wa klabu hiyo Ahmed Ally walitoa taarifa ya kumualika mtumishi Mwamposa kuwa miongoni mwa wageni maalumu ambao atahudhuria kwenye mchezo wao wa hatua ya robo fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika ambao watacheza dhidi ya klabu ya Al Masry.
Taarifa njema kwa Simba Sc ni kwamba siku ya leo jumapili tarehe 6 Aprilo, mtumishi Mwamposa amekiri kupokea mualiko huo na ameweka wazi kwamba yuko tayari kuungana na Simba Sc kwenye vita yao nzito dhidi ya waarabu yaani klabu ya Al Masry.
Mwamposa katika taarifa yake ameeleza wazi kwamba yeye kama mtumishi anabaki kuwa kiongozi wa timu zote kama vile Yanga Sc, Simba Sc, Azam Fc, Singida Black Stars na timu zote ambazo zinashiriki ligi kuu hivyo basi hawezi kugomea mualiko wake wa kwenda kuungana na Simba Sc kwenye mchezo huo.
Hii imekuwa taarifa njema sana kwa mashabiki na viongozi wa klabu ya Simba Sc kwa sababu maombi yao yamejibiwa kirahisi sana na mtumishi huyo ambaye kwa sasa amekuwa na msaada mkubwa sana kwa watanzania ambao wamekuwa na changamoto mbalimbali za kiafya na mambo mengine ya kimataifa.
From Opera News