Web

Hatimaye Ali Kamwe Aachiwa na Polisi Kwa Dhamana




Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ally Kamwe ameachiwa huru na jeshi la Polisi Mkoani Tabora

Ally Kamwe alishikiliwa na jeshi la Polisi kwaajili ya mahojiano ya masaa kadhaa kutokana tuhuma zilizokuwa zinamkabili juu ya kauli alizozitoa Aprili 1, 2025 juu ya viongozi wa Serikali kuelekea mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tabora United.

Taarifa zinaeleza kuwa Ally Kamwe alikamatwa majira ya saa 9, usiku wa kuamkia leo Aprili 3, na baada ya mahojiano ameachiwa huru

Dhamana inamruhusu kusafiri nje ya mkoa wa Tabora wakati Polisi wakiendelea na uchunguzi na ataripoti tena Aprili 21.

Msemaji huyu ameanza safari ya kurejea DSM

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad