Web

Hatimaye Kipa wa Fountain Gate Afukuzwa Baada Kufungwa na Yanga Kizembe




Kipa kutoka Nigeria John Noble ambaye ni kipa wa timu ya Fountain Gate na timu ya taifa ya Nigeria amefukuzwa kwenye klabu hiyo baada ya makosa ya wazi kwenye mchezo wa leo dhidi ya Young Africans.

Habari za uhakika zinasema kuwa Noble aneshaondolewa kambini na hayupo na wenzie. Aliondoka kiwanjani baada tu ya kufanyiwa mabadiliko huku wenzie wakitaka Kumpiga kwa makosa hayo ya kijinga.

Aidha Kocha Mkuu wa klabu ya Fountain Gate ametema cheche baada ya mechi ya leo na kudai kuwa mchezaji huyu alisababisha wao kupokea kichapo kikali cha mabao 4-0 dhidi ya Young Africans leo. Kulingana na taarifa tulizozipata hivi sasa Kocha Mkuu wa klabu ya Fountain Gate, Robert Matano alizungumza na waandishi wa habari mara tu baada ya mechi ya leo ya Fountain Gate dhidi ya Young Africans kukamilika.

Alisema kuwa golikipa wao aliwaangusha kabisa. Alieleza kuwa golikipa alifanya makosa mengi ambayo yalisababishwa kupata kichapo kikali. Jambo ambalo huenda likawa pigo kubwa kwa mchezo huyo.

Nikinukuu maneno ya kocha mkuu wa klabu ya Fountain Gate: Golikipa wa leo ametuangusha kabisa yaani golikipa wa aina yake kufanya makosa kama yale sasa kama tunacheza vizuri halafu tunapeana mabao vile itakuwa vigumu kushinda.

Kwa hiyo kwa msimamo wake amemrushia lawama mchezaji huyo na kudai kuwa yeye ndiye aliyesababisha wao kufungwa mabao mengi dhidi ya Young Africans leo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad