Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo @chadematzofficial, John Heche, leo Aprili 6, 2025, akizungumza na wakazi wa Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara amewaambia CHADEMA haiogopi uchaguzi ila wanataka mabadiko ya kimsingi ili uchaguzi uwe huru na wa haki.
"Mimi Heche niogope uchaguzi kweli? Dkt. Slaa anajua nimeanza kugombe nikiwa mwaka wa pili Chuo Kikuu, pale kwetu Tarime ni CHADEMA ni kama dini kila uchaguzi tulikuwa tunawapiga mpaka walipoanza kutuibia, ndio maana tunasema (No Reform no Election)"