Anaandika ✍️
@cheyolutenganotz
Kibu Denis anaisaka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa michuano ya kombe la shirikisho ikiwa anahitaji goli 2 kwenye mchezo ujao ili kumfikia kinara wa sasa.
Ismail Belkacemi kutoka Usm Alger ndiye anaongoza akiwa tayari amefunga magoli 5 moja likiwa kwa mkwaju wa penalti.
Ismail tayari ameondoshwa na timu yake hivyo hana uwezo wa kuongeza goli nyingine za ziada
Anayeshika nafasi ya pili ana magoli manne (4) Ifeanyi Ihemekwele wa Enyimba United ambaye pia aliyolewa kwenye michuano.
Kibu Denis ana nafasi kubwa ya kuwa kinara ukizingatia factor zifuatazo........
Waliopo juu yake wote wameondolewa kwenye michuano hivyo kazi kwake ni kufunga pekee.
Kibu Denis anakutana Stellenbosch ambao safu yao ya ulinzi inavuja kwa kiasi kikubwa imeruhusu mabao 10 kwenye hatua ya makundi yenye mechi 6 pekee
Kwenye ligi wameruhusu magoli 17 katika michezo 20 na kenda.
Kibu anaweza kufunga nyumbani na ugenini kwa kuwa tayari ameonyesha kiwango bora hata mechi za ugenini rejea mchezo dhidi ya Fc Bravos ambao alikuwa mchezaji bora wa mchezo kitu ambacho wenzake hawafanyi hivyo.
Wafungaji wengi wanafunga magoli wakiwa kwenye mechi za nyumbani mfano kinara mwenye goli 5 alifunga goli zote akiwa nyumbani
Vs Oropa United goli 2
Vs Asec Mimosas goli 2
Vs Diaraf goli 2
Lakini hajafunga wala kuwa mchezaji hatari kwenye michezo ya ugenini.
Kitu ambacho Kibu Denis pia amefanya zaidi ya wao rejea mchezo dhidi ya Cs Constantine na Cs Sfaxien bayo michezo yote alikuwa mchezaji bora
Faida ya Kibu ni kuwa Ismail licha ya kuwa kinara alishindwa kuwafunga Constantine ambao waliwaondoa Usm Alger lakini Kibu Denis aliwafunga na alikuwa mchezaji bora wa mchezo