Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amekamatwa na Jeshi la Polisi alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara eneo la Kariakoo jirani na soko jipya la vyakula.
Kwa mujibu wa taarifa baada ya kuanza kuhutubia kwa takriban dakika tano, Polisi walifika na kumtaka aache kuhutubia, ndipo ikatokea vuta nikuvute kati ya Polisi na wafuasi wa Chadema iliyodumu kwa dakika 30, hata hivyo wafuasi wa chama hicho walisema kama Polisi wanamuhitaji, watampeleka wenyewe kituoni.