“Viongozi wanapelekewa maelekezo kwamba Mtu yoyote ambaye yupo G55 anzeni kumwandikia barua na tumeshaona mmoja ameandikiwa Asenga, tunakishauri Chama chetu njia hiyo sio sahihi, tulipinga udikteta, tunaendelea kupinga udikteta ndani na nje ya Chama, tunawashauri Viongozi wetu wanaohubiri uhuru wa mawazo na maoni”
“Mwenyekiti (Lissu) alikuwa Mbunge, Makamu Mwenyekiti (Heche) alikuwa Mbunge, Katibu Mkuu (Mnyika) amewahi kuwa Mbunge, ndani ya Bunge walikuwa na maoni ya moto kwelikweli walipotaka kuzuiwa na Spika, kupewa adhabu, kutolewa nje ya Bunge tulisimama kama Taifa kwamba maoni yao yasikilizwe, na ndani ya CHADEMA leo tunawataka Viongozi wasiogope kusikiliza maoni mbadala”
“Watu waachwe wawe huru, kama CHADEMA tukianza kuzuia Watu wetu kusema hivi mnataka Wananchi wakasemee wapi?, hatutaki kuiga tabia za CCM, kwamba Mwanachama alihoji yule Malisa kwamba uteuzi wa Mgombea Urais haukufuata Katiba ya Chama wakaagiza Wilaya imfukuze uanachama, hivyo vimelea tunaona vinataka kuja CHADEMA, tunawasihi Viongozi wetu wasikubali hayo majaribu” —— John Mrema akiongea kwa niaba ya G55 Jijini Dar ess salaam April 06,2025