Kesi mbili za jinai zinazomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa Tundu Lissu zinatarajiwa kusikilizwa leo kwa njia ya mtandao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam
Kesi ya kwanza, ya uchochezi, yenye namba 202504102000008606, inasikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Geofrey Mhini ambapo imepangwa kwa usikilizaji wa awali leo, Aprili 24, 2025 saa tatu asubuhi
Kesi ya pili, ya uhaini, yenye namba 202504102000008607, inasikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Franco Kiswaga na imepangwa kwa kutajwa leo saa tano asubuhi, pia kwa njia ya mtandao.