Web

Kesi ya Nicole Bado Ngoma Ngumu, Haya Ndio Yaliyojiri...




Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni imeahirisha kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili msanii wa uigizaji Joyce Mbaga (32), maarufu Nicole Berry na mwenzake Rehema Mahanyu (31), hadi Mei 13, 2025 kutokana na upelelezi kutokamilika.

Kesi ya Nicole imeitishwa leo Aprili 14, 2025 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ramadhan Rugemalira kwa ajili ya kutajwa.

Wakili wa Serikali, Rhoda Maingu alieleza mahakama hiyo kuwa upelelezi wa shauri bado haujakamilika, hivyo anaomba ahirisho la kesi hiyo, ambapo imeahirishwa hadi Mei 13, 2025 kwa ajili ya kutajwa.

Kwa mara ya kwanza washtakiwa hao walifikishwa Mahakamani Machi 10, 2025 na kusomewa kesi ya uhujumu uchumi yenye mashitaka matatu likiwemo la kuongoza genge la uhalifu ambapo Wakili wa Serikali, Rhoda Maingu aliwasomea mashitaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ramadhani Rugemalira.

Katika mashitaka yao, washtakiwa hao wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Julai 2024 na Machi 2025 ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam. Washtakiwa wanakabiliwa na mashitaka matatu la kwanza la kuongoza genge la uhalifu.

Ikumbukwe kuwa Machi 17, 2025 Nicole aliachiwa huru kwa masharti ya dhamana ambapo amedhamiwa kwa hati ya nyumba yenye thamani ya Shilingi milioni 100 iliyotolewa na mmoja wa mdhamini wake, ambao hata hivyo majina yao hayajafahamika.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad