Kuelekea kwenye mchezo wao wa mkondo wa pili michuano ya Klabu Bingwa Afrika, klabu ya Fc Pyramids imekutana na sintofahamu nchini Morocco, baada ya kukosa uwanja wa kufanyia mazoezi kufuatia kunyimwa kutumia viwanja zaidi ya vinne walivyoomba bila maelezo ya kueleweka.
Baada ya kukwama, Pyramids aaliomba kutumia uwanja wa wenyeji wao, As Far Rabat ambao waliwaruhuzu, lakini walipofika kiwanjani hapo wakazuiliwa na wanajeshi waliokuwepo katika uwanja huo.
NB: KUMBUKA WAPINZANI WA PYRAMIDS FC KWENYE MCHEZO HUO NI AS FAR RABAT AMBAYO NI TIMU YA JESHI NCHINI MOROCCO, NA WALIIBUGIZA MABAO 4-1 KWENYE MCHEZO WA MKONDO WA KWANZA.