Klabu ya Leicester City inayonolewa na Ruud Van Nistelrooy imeshuka daraja rasmi kutoka Ligi Kuu England kwenda Ligi ya Championship England kufuatia kipigo cha 1-0 nyumbani dhidi ya Liverpool.
Kwa upande mwingine majogoo ambao wamefikisha pointi 79 kwenye msimamo wa Ligi wamezidi kuusogelea ubingwa wa Ligi hiyo ambapo wanahitaji kushinda mechi moja tu kutangazwa kuwa Mabingwa wa Ligi Kuu England kwa mara ya 20 kihistoria.
FT: Leicester City 0-1 Liverpool
⚽ 76’ Alexander-Arnold