Web

Kocha Al Masry Adai Mukwala na Ellie Mpanzu Walikuwa Mwiba Kwao...



Kocha mkuu wa Klabu ya Al Masry Boujelbene amesema baada ya mchezo wa kwanza walijipanga kuhakikisha wanamdhibiti winga Elie Mpanzu ambaye aliwapa wakati mgumu lakini hawakufanikiwa zaidi ya kuwaumiza kwa kufunga bao la kwanza huku akishtushwa na sapraizi ya mshambuliaji Steven Mukwala aliyefunga bao la pili wakiwa wamejiandaa kumkabili Leonel Ateba.

“Kule nyumbani yule kiungo wa pembeni jezi namba 34 (Mpanzu) alijituma sana tukasema tunatakiwa kumchunga hapa ugenini lakini hatukufanikiwa, ana nishati sana na nguvu za miguu.

“Wana mshambuliaji mzuri pia, unajua tulitegemea kumkabili Ateba (Leonel), mimi binafsi namfahamu lakini tulishangaa kumuona yule aliyefunga bao la pili (Mukwala) hata kwenye mechi nyingi tulizozifuatilia hatukumuona sana lakini bado na yeye akafanya vizuri.

“Nadhani wana timu nzuri ambayo inaweza kutenegeneza matokeo ndani ya dakika 90 lakini pia hata ukifika nao kwenye penalti wanaweza kufanya vizuri,” alisema Kocha huyo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad