Kupitia chombo cha habari cha TV3, Alex Ngereza amedai kuwa "Kocha wa Simba Club, David's amekiuka misingi ya ufundishaji kwasababu Jean Charles aliomba kufanyiwa mabadiliko lakini bado alimrudisha uwanjani kitu ambacho sio sawa. Katika sheria za ualimu wa soka mchezaji akiomba mabadiliko basi anatakiwa atolewe haraka sana".
Aliendelea na kusema kuwa, "Hata kama mchezaji ni muhimu kwenye kikosi lakini akiomba kufanyiwa mabadiliko, maana yake hawezi tena kuendelea na mchezo anapaswa kubadilishwa. Fadlu david alipaswa kumtoa Jean Charles na kama umeangalia vizuri hata baada ya kumrudisha uwanjani bado alikuwa anachechemea na kuonyesha kwamba misuli inamsumbua.
Mbali na apo Alex Ngereza alizungumzia pia kuhusu sheria za mpira na majeraha kwa mchezaji ambapo alisema kuwa, hata kisheria za mpira mchezaji haruhusiwi kutumika akiwa na majeraha". Hivyo basi, Fadlu David's alikosea sana kumbakisha Ahoua wakati mwenyewe anadai kutoka.
Ikumbukwe ya kwamba, katika mchezo huo Simba waliibuka washindi wa bao moja kwa sifuri dhidi ya Stellenbosch FC, katika mcheoz wa nusu fainali raundi ya kwanza. Ambapo, mzunguko wa pili unaenda kupigwa huko Afrika Kusini na mshindi ataenda Fainali.
Je unaamini kuwa Simba itaingia fainali au itaishia hapa hapa nusu fainali?. Tuandikie maoni yako hapo chini pia usisahau kugusa like na share asante.