Mayele na Inonga Bacca Uso Kwa Uso Leo Ligi ya Mabingwa Afrika
Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) inaendelea kutimua vumbi leo Aprili 01, 2025 kwa michezo ya mkondo wa kwanza wa hatua ya robo fainali ambapo Mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri watatupa karata yao nyumbani dhidi ya Al Hilal ya Sudan.
Wababe wa Afrika Kusini, Mamelodi Sundowns watakuwa wenyeji wa Esperance ya Tunisia huku MC Alger wakiwa wenyeji wa Orlando Pirates.
Beki wa zamani wa Simba Sc, Henock Inonga Baka na mshambuliaji wa zamani wa Yanga Sc, Fiston Mayele watakutana uso kwa uso wakati Pyramids ya Mayele wakiikaribisha FAR Rabat ya Inonga.
16:00 Sundowns 🇿🇦 vs 🇹🇳 Esperance
22:00 Ahly 🇪🇬 vs 🇸🇩 Al Hilal
22:00 Pyramids 🇪🇬 vs 🇲🇦 FAR Rabat
16:00 MC Alger 🇩🇿 vs 🇿🇦 Pirates