Web

MBOWE Amjulia Hali Tundu Lissu, Waongea Kwa Saa Moja Gerezani....

MBOWE Amjulia Hali Tundu Lissu, Waongea Kwa Saa Moja Gerezani....


Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mhe. @freemanmbowetz akiambatana na Salum Mwalimu aliyekuwa Naibu katibu Mkuu wa Chama hicho Zanzibar pamoja na Daniel Naftal Ngogo, mwandani wa karibu wa kiongozi huyo Mstafu wa Chadema wamefika gereza la Keko Jijini Dar Es salaam na kumjulia hali Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe. @tunduantiphaslissu leo Jumatano Aprili 16, 2025, majira ya saa sita Mchana.

Chanzo chetu cha habari kilichowanasa viongozi hao wakiwa kwenye mazungumzo, kimeeleza kuwa wawili hao wamefanya mazungumzo kwa muda wa takribani saa moja, wakijadili na kuzungumza masuala mbalimbali.

Lissu Aprili 10, 2025 alirudishwa mahabusu baada ya kusomewa shitaka la uhaini katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kufuatia kushindwa kujitetea kutokana na kosa hilo kumnyima dhamana na nafasi ya kujitetea, akituhumiwa pia kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao wa kijamii wa X akitarajia kupandishwa tena mahakamani Aprili 24 mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad