Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Aida Kenani ameitaka serikali kuanza kufikiri na kupanga mikakati mbalimbali ya Tanzania kuondokana na utegemezi kutoka nje ya nchi, akikosoa matumizi makubwa ya fedha zinazotumika kwaajili ya ununuzi wa Magari ya gharama kubwa na yasiyoendana na mazingira Halisi yanayotumiwa na Wakuu wa Wilaya.
Aida kadhalika ameitaka serikali kutojisifu na Ujenzi wa miundombinu ikiwemo majengo kwenye sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya afya na elimu, badala yake ni Jukumu la Bunge kuhoji ubora wa huduma zinazotolewa kwenye majengo hayo ikiwa zinakidhi matarajio ya wananchi wa Tanzania.
Mhe. Kenani ameshauri kuwa kama Bunge ni muhimu kuwasaidia wananchi kwa kusimama kidete kuhoji na kuisimamia serikali ili iweze kutimiza majukumu yake kikamilifu kwa wananchi.