Web

Mchakato wa Ubunge, Udiwani na Uwakilishi CCM Kuanza Mei Mosi

Mchakato wa Ubunge, Udiwani na Uwakilishi CCM Kuanza Mei Mosi


Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewatangazia Wanachama wake kwamba, mchakato wa ndani ya Chama wa uteuzi wa wagombea nafasi za Ubunge, Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi na Udiwani, kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025, utaanza rasmi tarehe 1 Mei, 2025 kwa zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu za maombi ya kuteuliwa kugombea nafasi hizo.


Taarifa ya leo Aprili 10, 2025 iliyotolewa na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla, Taifa imeeleza kuwa zoezi hilo litaanza tarehe 1 Mei, 2025, saa 2:00 asubuhi na kumalizika tarehe 15 Mei, 2025, saa 10:00 jioni ambapo utaratibu wa kuchukua na kurejesha fomu za maombi utakuwa kama ifuatavyo:-


a) Wanachama wanaogombea nafasi ya Ubunge au Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi watachukua na kurudisha fomu kwa Katibu wa CCM wa Wilaya inayohusika.


b) Wanachama wanaogombea nafasi za Viti Maalumu vya wanawake katika Bunge au Baraza la Wawakilishi, kupitia kundi la UWT pamoja na makundi maalumu (NGOS, WAFANYAKAZI, WASOMI na WALEMAVU) watachukua fomu na kurudisha kwa Katibu wa UWT wa Mkoa unaohusika.


c) Wanachama wanaogombea nafasi za Viti Maalumu vya wanawake katika Bunge au Baraza la Wawakilishi kupitia jumuiya ya UVCCM watachukua na kurudisha fomu kwa Katibu wa UVCCM Mkoa unaohusika.


d) Wanachama wanaogombea nafasi za Viti Maalumu vya wanawake katika Bunge au Baraza la Wawakilishi kupitia jumuiya ya WAZAZI watachukua na kurudisha fomu kwa Katibu wa WAZAZI Mkoa unaohusika.


e) Wanachama wanaogombea nafasi ya Diwani wa Kata (Bara) au Wadi (Zanzibar) watachukua na kurudisha fomu kwa Katibu wa CCM wa Kata/Wadi inayohusika.


f) Wanachama wanaogombea nafasi ya Udiwani Viti Maalumu vya Wanawake watachukua na kurudisha fomu kwa Katibu wa UWT wa Wilaya inayohusika.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad