Mjadala umeibuka kati ya #DivaTheBawse na #Lukamba, aliyewahi kuwa mpiga picha wa #DiamondPlatnumz – kuhusu maisha baada ya kuondoka kwenye lebo ya Wasafi (WCB). Diva alimkumbusha Lukamba umuhimu wa kuwa na shukrani kwa Diamond kwa nafasi aliyompa, akisema alimsogeza mbali, ikiwemo kumfikisha kwenye jukwaa la kimataifa. Alisisitiza kuwa hata kama kuna changamoto, si vyema kuongelea vibaya watu waliokusaidia.
Lukamba kwa upande wake alieleza kuwa si kila mtu aliyepita Wasafi alinufaika ipasavyo. Alisema baadhi ya watu walipoondoka ndipo walipojipata na kupata mafanikio ambayo hawakuwa nayo awali. Alitoa mfano wa dancers waliotimkia Marekani, na bodyguard Mwarabu Fighter ambaye alisema maisha yalikuwa magumu alipokuwa chini ya Diamond.
Tunaweza kuona mifano mingine
Harmonize aliondoka Wasafi na kuanzisha Konde Gang, akafanikiwa kuendelea kuwa mmoja wa mastaa wakubwa.
Rayvanny naye alifungua Next Level Music na anaendelea kufanya Kazi zake, akiwa na uhuru wa kisanii, wakosoaji wanasema bado anaishi kwenye mfumo wa Wasafi
Rich Mavoko alilalamikia kusaini mikataba ya kinyonyaji iliyomnyoma uhuru alipokuwa WCB. Alipoondoka, alijitahidi kujisimamia lakini hajafanikiwa kwa kiwango kikubwa.
Baadhi ya dancers waliokuwa Wasafi sasa wanaishi Marekani na kufanya vizuri kwa kujitegemea.
Mwarabu Fighter, aliyekuwa bodyguard wa Diamond, alisema alikuwa na madeni na maisha magumu alipokuwa Wasafi.
Hii inaonesha kwamba kila mtu ana ukweli wake. Wapo waliothamini nafasi waliyopewa ndani ya Wasafi, lakini pia wapo waliopata nafasi zaidi walipoondoka. Wengine walipanda, wengine walipotea.
Kwa hiyo, mjadala huu unagusa vipengele viwili muhimu:
Shukrani kwa fursa uliyopata.
Uhalisia wa maisha ndani ya hiyo fursa.
Je, mafanikio ya kweli yanatokana na kuwa sehemu ya jina kubwa au uwezo binafsi wa kupambana nje ya mfumo huo? Ukweli uko katikati, kila mtu ana hadithi yake.
✍️: @enkyfrank