Mwanariadha wa Tanzania Alphonce Felix Simbu, ameshika nafasi ya pili kwenye mbio za Boston Marathon zilizofanyika leo Aprili 21, 2025 Masachusetts nchini Marekani na kujinyakulia zawadi ya Shilingi Milioni 201.4
Simbu alikimbia kilomita 42 na kumaliza mbio hizo kwa muda wa saa 2:05:04, akiwapita wanariadha wengi waliokuwa wakipewa nafasi kubwa ya kushinda Katika mashindano hayo yaliyohusisha wanariadha mahiri kutoka mataifa mbalimbali duniani.