Nashangaa bado kuna Vijana wanaamini mapenzi siyo pesa, wakati mnajionea wenyewe namna Zuchu na Rita wanavyomgombania Diamond kisa pesa na umaarufu alionao. Tungerudi miaka 15 nyuma enzi za Nitarejea, Mbagala, Zuchu na Rita wangeweza kuumiza vichwa vyao kumgombania Diamond? jibu ni hapana wanamgombania kwa sababu ya Pesa.
Madhara ya Wanawake kufata Wanaume wenye hela ni kwamba Mwanaume hatokupenda kwa dhati bali atakuwa na wewe kwa ajili ya kupata utamu tu, ndio maana unaweza ukaona vita yote inayoendelea kati ya Zuchu na Rita, Diamond Platnumz hajaongea chochote, hajamtetea Zuchu wala Rita maana anaamini wote ni wanafiki, wanagombania pesa zake tu.
Nina uhakika Diamond alimpenda sana Wema Sepetu kwa sababu walikutana akiwa bado hana kitu lakini Wema akakubali kuwa naye, hapa Bongo angalau Mwanamke mwenye mapenzi ya kweli ni Wema maana anaweza ku-date na wewe hata kama huna kitu, mpaka sasa unaweza ona anatoka na Whozu ukashangaa, lakini hata alivyoanza kutoka na Diamond Platnumz, Simba hakuwa na maisha mazuri kama aliyonayo sasa.
Mnajiuliza sana kwanini Diamond Platnumz alimpenda sana Sarah, jibu ni kwamba Mwanamke huyo alikubali kuwa naye enzi hizo maisha ni magumu lakini akavumilia, hivyo mpaka sasa Diamond sio mjinga anajua kabisa kuanzia Mobetto, Zari, Tanasha, Zuchu, Rita hakuna anayempenda kwa dhati, bali wanapenda hela tu, ndio maana huwa ni rahisi wao kujitegesha wapate mimba, angalia kuanzia Mobetto, Zari, Tanasha ilikuwa jambo rahisi kumzalia Diamond, huyu Rita naye alishapata Mimba ya Diamond ila ikaharibika, bado Zuchu tu kupata mimba na nashangaa mpaka sasa sijui kwanini hajategesha apate mimba ili aendelee kupata Child Support.
Hivi mnadhani kwanini katikati ya vita ya Zuchu na Rita Diamond ame-post kuwa Vocha yake kwenye simu ni zaidi ya Milioni 9, pia ameichoka Rolls Royce yupo njiani kuleta Chuma kipya Bugatti? hii anaonesha makusudi kuwa pesa anayo ndio maana Mabinti kama Zuchu na Rita wapo tayari kujidhalilisha mitandaoni ilimradi kila mmoja apendwe zaidi na Diamond.
SOMO LA LEO! WANAUME TUTAFUTE HELA, TUWE HURU KWENYE UHUSIANO NA TUAMUE YUPI WA KUOA, YUPI ANA TAMAA TU, HIVYO ANAFAA KUCHEZEWA TU