Web

Nabi Aipa Silaha SIMBA Kuiuwa Stellenbosch Amani Complex

Top Post Ad

Nabi Aipa Silaha SIMBA Kuiuwa Stellenbosch Amani Complex


KUNA sababu tatu ambazo kocha wa zamani wa Yanga SC Nasreddine Nabi amezitaja ambazo zinaipa Simba SC nafasi kubwa ya kuitoa Stellenbosch ya Afrika Kusini.

Nabi ambaye kwa sasa anaifundisha Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, amesema anawafahamu vizuri Stellenbosch kwani hivi karibuni amecheza nao mara tatu na kuwapiga nje ndani.

Kocha huyo raia wa Tunisia, katika mechi hizo tatu alizocheza dhidi ya Stellenbosch na kushinda zote, mbili za Ligi Kuu Afrika Kusini na moja Kombe la Nedbank hatua ya robo fainali.

Akizungumza na Mwanaspoti, Nabi aliyeifundisha Yanga kuanzia Aprili 20, 2021 hadi Juni 15, 2023, alisema tangu afike Afrika Kusini na kuanza kuifundisha Kaizer Chiefs kuanzia Julai Mosi 2024 amekutana na Stellenbosch mara tatu na kubaini ni timu isiyotabirika ikiwa na kikosi kizuri.

Nasreddine Nabi × Mwanaspoti

Below Post Ad

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.