Web

Rais Samia Ataja Reforms Zilizofanyika Kuelekea Uchaguzi

Rais Samia Ataja Reforms Zilizofanyika Kuelekea Uchaguzi

Rais Samia Ataja Reforms Zilizofanyika Kuelekea Uchaguzi

 Tukiwa tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu (2025), serikali imesema itahakikisha inashughulikia changamoto na kasoro zilizojitokeza kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwaka uliopita (2024) ili zisijitokeze kwenye chaguzi zijazo.


Ahadi hiyo imetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan @samia_suluhu_hassan wakati akihutubia kwenye Baraza la Eid El-fitr kitaifa, hafla iliyofanyika jioni ya leo, Jumatatu Machi 31.2025 kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.


Katika maelezo yake Rais Dkt. Samia amesema hata hivyo kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu (2025) mabadiliko makubwa yamefanyika kwenye sheria zinazosimamia uchaguzi huo, ikiwemo kuanzishwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) ambayo ilikuwa kilio cha muda mrefu nchini, kuondoa utaratibu wa Madiwani na Wabunge kupita bila kupingwa nk

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad