Web

Serengeti Boys Yaanza Vibaya AFCON U-17, Yachapwa 4-1

Serengeti Boys Yaanza Vibaya AFCON U-17, Yachapwa 4-1

Matokeo Serengeti Boys  Vs Zambia AFCON U-17 

Serengeti Boys imepokea kichapo cha mabao 4-1 kutoka kwa Zambia katika mechi ya kwanza ya kundi A kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON) inayoendelea Morocco.

Jonathan Kalimina aliipatia Junior Chipolopolo bao la kuongoza baada ya dakika 8 pekee kwenye Uwanja wa El Bachir, Mohammedia.

Nahodha Kassim Juma wa Tanzania na wachezaji wenzake walijaribu kujipanga upya na kuanza kutengeneza nafasi za mbele kupitia kwa Jabiri Farijala na Juma Abushiri.

Lakini kabla ya muda, Abel Nyirongo aliifungia Zambia bao na kipindi cha kwanza kumalizika ikiwa 2-0 baada ya kuunganisha krosi nzuri kutoka kwa Nthasilwe Malupande.

Baada ya mapumziko, Tanzania ilirejea ikiwa imechangamka na kudhamiria kupata mabao kwa kuwa shuti la Juma Sagwe liliokolewa.

Bao la kufutia machozi la Tanzania lilikuja kufungwa kupitia kwa mchezaji Sagwe kwa kichwa na kumshinda kipa wa Zambia Rogers Simumba.

Tanzania itarejea dimbani siku ya Alhamisi dhidi ya Uganda. Uganda ilipoteza mechi ya kwanza ya Kundi A kwa mabao 5-0 na wenyeji Morocco Jumapili usiku.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad