Web

Simba Bado Hawajamkubali Ahoua...Wataka Chenga Kama za Pacome



Simba Bado Hawajamkubali Ahoua...Wataka Chenga Kama za Pacome

Simba Bado Hawajamkubali Ahoua...Wataka Chenga Kama za Pacome


“Nimemtazama Jean Charles Ahoua vizuri tu. Ni kiungo mzuri wa matukio. Anafunga, anapiga penalti vizuri. Anapiga mipira ya adhabu vyema. Lakini hajaumbwa kiungo mtawala dimbani. Wazungu kwa kile Kiingereza chao huwa wanaita dominant midfielder.

Dominant midfielder ni kiungo anayegeuka, anaondoka na mpira, anaweza kugeuka tena na tena, kisha akaachia nafasi na hapo hapo akapokea tena mpira na kupiga pasi rula kwenda eneo la adui. Kiungo mtawala huku uswahilini kwetu lazima awe na udambwiudambwi. Licha ya kugeuka na kupita katikati ya watu inabidi awe na chenga za madaha, tobo kidogo na kanzu ikibidi.

Ahoua sio kiungo wa namna hii. Ni kiungo anayecheza kwa msingi wa matukio. Nimepata habari za ndani namna ambavyo kuna mabosi wa Simba hawaridhiki naye. Wangefurahi kuwa na Feitoto kuliko Ahoua. Wanadai amefunga mabao rahisi, pia asisti zake ni zile za kupiga friikiki zinazotumiwa vyema na washambuliaji wake.

Kwa mpira wetu inakuwa NGUMU kumkubali kiungo kama Ahoua. Hachezi kama namba 10 inavyotakiwa kuchezwa kwa mujibu wa viwango vyetu vya mpira. Kwamba namba 10 lazima ndio awe staa wa timu. Kiongozi wa akili za wachezaji waliopo uwanjani.

Ninavyojua kwa namna watu wa Simba wasivyoridhika sana na Ahoua licha ya namba zake kuwa vyema, ni kwamba kwa sasa lazima wawe sokoni kuendelea kumsaka namba 10 aina ya Pacome. Labda ndiyo maana licha ya Ahoua kuwa na namba nzuri lakini bado Simba hawajaacha kumuota Fei.”

— Edo Kumwembe [via Mwnaspoti]

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad