Mwenyekiti wa klabu ya Simba Murtaza Mangungu anaamini kwa uwezo wa Mungu wanaenda kushinda mchezo wao dhidi ya Al Masry na kufuzu hatua ya Nusu Fainali ya kombe la Shirikisho Afrika.
"Sisi tunapambana na tunaamini kwa uwezo wa Mungu tutashinda. Jambo moja sisi hatutishwi na mtu.Wito wetu kwa Wanasimba kuiunga mkono timu yao kuelekea mchezo huo.
"Kwa kipekee tunamshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania pamoja na viongozi wengine kwa ushirikiano wanaotupatia katika maandalizi.”
- Murtaza Mangungu, Mwenyekiti wa Klabu ya Simba SC.