MIKATABA ya wachezaji watatu wa zawa ndani ya @simbasctanzania inaelekea ukingoni yupo golikipa aliyenamafanikio zaidi katika klabu ya simba kwa muda wote Aishi manula🙌 Yuko Mohamed hussen na Shomari kapombe.
Chaajabu mashabiki na wanachama wa SIMBA hawataki kusikia manula akiongeza kandarasi kuitumikia klabu ya simba ambayo ameitumikia kwa miaka takribani 11 na ameipambania nembo ya simba katika kukuza na kujenga ukubwa huu tunaouona KIMATAIFA katika ngazi ya klabu,Robo fainali mara 4 klabu bingwa afrika mwamba panga pangua.
Sitasita kumpa maua yake manula nikikumbuka alivyoikuta simba wakati anatokea Azam fc hakuna golikipa aliweza kumpoka namba yake sio kwa wazawa hadi wageni.
Mpaka leo sijui hasa kosa la manula Nini pale msimbazi nadhani ni wakati sahihi Sasa kuondoka akatafute changamoto mahali pengine ila tukumbule ww ukisema chann wenzako wanasema tutakipata lini.
UMETENDA MEMA MENGI AIR MANULA USINGOJE MALIPO ONDOKA ZAKO.