Web

Tundu Lissu Adaiwa Kugoma Kesi zake Kuendeshwa Mtandaoni

Tundu Lissu Adaiwa Kugoma Kesi zake Kuendeshwa Mtandaoni

Tundu Lissu Adaiwa Kugoma Kesi zake Kuendeshwa Mtandaoni

Imeelezwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa Tundu Lissu amegoma kesi yake ya uchochezi na uhaini kusikilizwa kwa njia ya mtandao leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam akidai kuwa hajawasilishwa rasmi mahakamani.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo rasmi vya chama hicho, Kesi ya uchochezi, yenye namba 202504102000008606, ilipangwa kwa usikilizaji wa awali leo saa tatu asubuhi mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Geofrey Mhini kwa njia ya mtandao

Hata hivyo, Lissu amekataa kuendelea na mchakato huo akisisitiza kuwa uwepo wake mahakamani ni muhimu, na kwamba hakufikishwa mahakamani kama inavyotakiwa kisheria.

Kesi nyingine ya uhaini inayomkabili, yenye namba 202504102000008607, nayo imepangwa kutajwa saa tano asubuhi mbele ya Hakimu Mkazi Franco Kiswaga, pia kwa njia ya mtandao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad