Web

UKWELI USEMWE: AZAM FC Sajili zao Kwa Asilimia Kubwa Zimefeli....

 

UKWELI USEMWE: AZAM FC Sajili zao Kwa Asilimia Kubwa Zimefeli....

AZAM SAJILI ZAO KWA ASILIMIA KUBWA ZIMEFELI.

📝Mwisho wa msimu uliopita hata kabla dirisha kubwa la usajili halijafunguliwa Azam walianza kufanya sajili kwenye klabu yao hasa za wachezaji wa kimataifa na kwa Azam walianza na wachezaji raia wa Colombia wengi walikuwa na matumaini na sajili hizo.


📝Hata wakati wa dirisha kubwa bado viongozi wa Azam walikuwa bize sana kufanya sajili kwani walikuwa wawakilishi wa nchi kwenye CAF Champions league hivyo walikuwa kwenye wakati wa kujenga timu ya ushindani.


📝Sajili zilikuwa nyingi na karibia kila position walisajili kitu ambacho matarajio yalikuwa mengi kwa Azam msimu huu,Kwanza wengi walidhani watafanya vizuri CAF Champions league na hata kwenye ligi lakini yote yameenda tofauti.


📝CAF Champions league hatua za awali tu waliondoshwa kwenye ligi kuu napo mambo yameshakuwa magumu kutoka kumaliza top two msimu uliopita hadi kuanza kuipambania top four msimu huu kitu ambacho ni big disappointed kwa fans wa Azam Fc.


📝Kwenye kombe la CRDB federation Cup napo wameondoshwa mapema licha ya misimu kadhaa kucheza fainali na nusu fainali ila awamu hii kwao imekuwa ngumu baada ya kutolewa na Mbeya city.


📝Hakuna mchezaji ambaye amekuwa surprise pale Azam kwa sajili zilizofanywa msimu huu ni yuleyule FEISAL SALUM ambaye bado ndio anabaki kuwa most valuable player kwenye kikosi cha Azam kutoka na ubora wake na consistency yake kwenye kikosi cha Azam

By Hansrafael

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad